Akina mama 700 hadi 1, 000 wanafika kujifungua kila mwezi katika kituo cha afya cha Katoro Mamlaka ya mji mdogo wa Katoro halmashauri ya wilaya ya Geita.
Akina mama wengi wamekuwa wakifika katika kituo hicho cha afya, kutokana kuboreshwa kwa huduma za afya kituoni hapo.
Maeneo yaliyoboreshwa ni pamoja na ujenzi wa wodi mpya ya akina Mama, jengo la upasuaji na vifaa vyake, na kwa sasa kuna dawa za kutosha.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mganga Mkuu Mfawidhi wa kituo hicho cha afya cha Katoro Dkt. Zakaria Nyerere baada ya kupokea msaada uliotolewa na mgodi wa dhahabu wa Buckreef pamoja na chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU), msaada uliotolewa kwa akina mama wajawazito na wale waliojifungua katika kituo hicho cha afya.
Amesema kutokana na maboresho yaliyofanyika katika kituo hicho cha afya kati ya wanawake 50 na 70 wamekuwa wakifanyiwa upasuaji, tofauti na hapo awali ambapo walikuwa wanapelekwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita.
Meneja rasilimali watu wa mgodi wa dhahabu wa Buckreef, Imelda Msuya amesema ni wajibu wa mgodi kusaidia jamii pale wanapoona kuna uhitaji.
Msaada uliotolewa na
mgodi huo wa dhahabu wa Buckreef pamoja kituo cha afya cha Katoro ni pamoja na sukari kilo 160, dawa za kufanyia usafi, madaftari, sabuni, taulo za watoto na taulo za kike.