Yanga: Tupo tayari kumuuza Fei Toto

0
368

Yanga SC imekataa ombi la Feisal Salum la kutaka kuvunja mkataba na kumtaka mchezaji huyo arejee kambini haraka iwezekanavyo na kuendelea kuutumikia mkataba wake kama mchezaji halali wa klabu hiyo.

“Klabu ya iko tayari kumpokea Feisal Salum na kumjumuisha kwenye kikosi, na kwa kuzingatia sera na utaratibu wa Klabu ya Yanga katika kuwaongezea mikataba wachezaji wake wanaofanya vizuri, uongozi wa Yanga uko tayari kuendelea na mazungumzo na Feisal Salum na wawakilishi wake juu ya kuboresha mkataba wake kama wataridhia,” imesema taarifa hiyo.

Aidha, klabu hiyo imesema iko tayari kumruhusu mchezaji huyo kuondoka klabuni hapo kwa kuzingatia matakwa ya mkataba na utaratibu wa sheria za uhamisho wa wachezaji zinazotambulika na TFF pamoja na FIFA.

Pia imesema kuwa ikiwa kuna klabu yoyote inahitaji huduma ya mchezaji huyo, Klabu ya Yanga  iko tayari kufanya mazungumzo wakati wowote.