CCM yataka ukarabati wa barabara ya Orbesh – Haydom

0
124

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amemuagiza meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoa wa Manyara kumuandikia barua Mtendaji Mkuu wa Wakala huo kutoa fedha za dharura kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Orbesh hadi Haydom wilayani Mbulu ambayo ni mbovu na imekuwa kero kwa wananchi.

Chongolo ametoa agizo hilo katika mkutano wake na wananchi wa kata ya Hydirir wilayani humo baada kujionea hali halisi ya barabara hiyo.

“Barabara hii haijanifurahisha ni mbovu hasa ikizingatiwa huku mnalima sana, sitaki mlete hadithi za masuala ya bajeti nataka barabara itengenezwe ipitike, sijaja hapa kupiga porojo nimekuja kuchukua changamoto zenu wananchi nihangaike nazo kupata ufumbuzi,” amesema Chongolo