Akijibu swali kuhusu ugumu wa kuanzisha vyombo vya habari vya mtandaoni , Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha amesema kuna sheria zilitungwa na kulikuwa na vikwazo kwa mtu kuanzisha blogu, Lakini sasa urahisi umeongezeka kwa kiasi kikubwa.
“Lazima tuwe na vijana ambao si wepesi wa kuangalia sana vikwazo, inakuwaje ndani ya vikwazo hivihivi tunapata vijana kama (na nitamtaja bila hofu), Millard Ayo. Nani alimpa mtaji Millard Ayo kuanzisha ile empire. Leo naona kijana mdogo alikuwa tu mtangazaji, ana magari yake na yanakimbia yanatafuta habari. Na yeye ni kijana aliyejiamini,” amesema Dkt. Rioba
Aidha, ameongeza kuwa, kuwa na uhuru ni suala moja na muhimu zaidi ni kujua namna bora ya kuutumia uhuru huo kwa ajili ya jamii inayokuzunguka.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.