Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano elekezi wa viongozi wa Serikali

0
279

WANAPOFIKA OFISINI MANENO YANAWARUDISHA NYUMA

“Tuepuke kauli zinazowafanya wawekezaji kutilia shaka dhamira ya Serikali. Tunapokwenda huko nje tunakwenda na lugha nzuri tumefanya hivi tumerekebisha hiki kuna hiki tunawaita njooni muwekeze kwetu wanakuja kwa wingi, wanapofika maofisini maneno wanayoyapata yanawarudisha nyuma.

Nataka niwaambie katika dunia hii ya utandawazi, dunia yenye mitandao likikutoka neno moja mwekezaji akilichukua na kuliweka kwenye mitandao huko ya kiulimwengu kulifuta hilo neno ni shida au kuifuta hiyo ‘impression’ [taswira] uliyompa ni shida na hiyo impression [taswira] inasambaa kwa haraka dunia nzima. Niwaambie sana ndugu zangu kuwa makini na kauli tunazizitoa.”

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN