Koffi ahukumiwa kifungo cha miaka miwili jela

0
1280

Nyota wa muziki wa mtindo wa rumba na soukous, -Koffi Olomide amepatikana na hatia ya udhalilishaji wa mmoja wa wanengeuaji wake, wakati mnenguaji huyo akiwa na umri wa miaka Kumi na mitano.

Mahakama moja nchini Ufaransa imemuhukumu mwanamuziki huyo nyota kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Afrika, mwenye umri wa miaka 62, kifungo cha miaka miwili jela kutokana na kutenda kosa hilo.

Olomide pia ameamriwa kulipa Euro 5,000 kwa mnenguaji huyo kutokana madhara aliyomsababishia kufuatia udhalilishaji huo.

Mahakama hiyo pia imemuamuru alipe faini ya Euro 5,000 kutokana na kitendo alichokifanya cha kuwasaidia wanawake watatu kuingia nchini Ufaransa kinyume cha sheria.