Lewandowski nje Barca vs Real Madrid

0
171

Robert Lewandowski ataikosa mechi ya El Clasico kutokana na majeraha nyuma ya paja aliyoyapata katika mchezo wa mwisho wa wiki dhidi ya Almeria.

HALI IKOJE? Barcelona imethibisha kwamba mshambuliaji huyo ni majeruhi na kwamba hakuna uhakika kwamba atakuwepo kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Copa del Rey dhidi ya Real Madrid utakaopigwa Alhamisi.

Mbali na raia huyo wa Poland ambaye ana magoli 25 kwenye mechi 21, Kocha Xavi atawakosa pia Pedri na Ousmane Dembele ambao watakuwa nje ya uwanja hadi katikati ya Machi.

NINI KINAFUATA? Baada ya Barca kuondolewa kwenye mashindano ya Europa League pamoja na kipigo kutoka kwa Almeria, vijana wa Xavi wanakwenda kukabiliana na washindani wao wa jadi, mchezo ambao unatarajiwa kutoa tafsiri ya ubingwa wa La Liga.