Maalim Seif ahamia ACT Wazalendo

0
455

Aliyekua Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad,  ametangaza kukihama chama hicho na kuhamia Chama Cha ACT Wazalendo.

Maalim Seif ametangaza uamuzi huo wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Uamuzi huo wa Maalim Seif umekuja siku Mbili tu baada ya Chama Cha Wananchi (CUF) kumchagua Khalifa Suleiman Khalifa kuwa katibu Mkuu wake mpya, kufuatia uchaguzi uliofanywa na Baraza Kuu la chama hicho.