UN Women kuendelea kuwainua wanawake

0
154

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake (UN WOMEN) limesema, litaendelea kushirikiana na wadau wanaosimamia haki za wanawake na usawa wa kijinsia.

Kauli hiyo imetolewa na Mwakilishi Mkazi wa UN Women Tanzania, Hodan Addou wakati wa maadhimisho ya miaka 15 ya Mfuko wa Udhamini wa wanawake Tanzania (WFT-T).

Addou amesema UN Women itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuwainua wanawake kwenye harakati zao za kujikwamua kiuchumi na kujiletea usawa wa kijinsia pamoja na maendeleo katika ngazi mbalimbali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa mfuko huo wa Udhamini wa Wanawake Tanzania,
Rose Marandu amewapongeza waanzilishi wa mfuko huo kwa jitihada zao za kushirikiana na serikali, sekta binafsi na mashirika ya haki za wanawake.