Mtumbwi wazama, watoto 4 hawajulikani walipo

0
206

watoto wanne hawajulikani walipo baada ya mtumbwi uliokuwa umebeba watoto sita wa shule ya msingi Kagera kuzama katika mto Ruiche kata ya Kagera manispaa ya Kigoma – Ujiji.

Nahodha wa mtumbwi huo Ndemeye Andrea amesema, ajali hiyo imetokea majira ya saa mbili asubuhi hii leo wakati akiwavusha watoto hao kwenda shule ambayo ipo eneo la ng’ambo.

Vikosi vya zimamoto na uokoaji vikiongozwa na mkuu wa wilaya ya Kigoma vinaendelea na juhudi za kuwatafuta watoto hao ambao hawajulikani walipo mpaka sasa.