Pedri na Gavi kuikosa Man United

0
252

Barcelona leo inaikabili Machester United katika Uwanja wa Old Tranford bila nyota wake wawili, Pedri na Gavi, mchezo ambao utakuwa na ushindani mkali kila timu ikiwa nafasi ya kusonga mbele.

Pedri anaukosa mchezo huo kutokana na kuwa na majeraha ya paja aliyoyapata katika mchezo uliopita na kumlazimu kutolewa dakika ya 40. Kwa upande wa Gavi anaukosa mchezo huo kutokana na kuwa na kadi tatu za njano.

Kuokana na kukosekana kwa nyota hao Frenkie de Jong atabebeshwa jukumu la kuongoza safu ya kiungo ya Barca.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Nou Camp timu hizo zilitoka sare ya magoli 2-2, hivyo atakayepoteza mchezo wa leo atakuwa ameaga mashindano hayo ya Europa League.