Augua ugonjwa wa kubadilika lafudhi

0
181

Mwanaume mmoja raia wa Marekani mwenye umri wa miaka 50 ambaye jina lake limehifadhiwa, ameripotiwa kupatwa na ugonjwa usiokuwa wa kawaida wa kuzungumza lafudhi ya kigeni.

Mwanaume huyo alijikuta akizungumza kwa lafudhi isiyoweza kudhibitiwa ambayo ni ya Irish, baada ya kugundulika kuwa na tenzi dume na aliendelea kupatwa na tatizo hilo hadi alipofariki dunia.

Ugonjwa huo ulifanyiwa uchunguzi na kuripotiwa na chuo kikuu cha Duke katika jimbo la North Carolina pamoja na chuo kingine cha utafiti wa Urolojia Kusini mwa Carolina.

Mwanaume huyo aliugua ugonjwa wa lafudhi ya kigeni unaojulikana kama FAS, ugonjwa unaoelezwa kuwa wa nadra ambao humfanya mtu azungumze kwa lafudhi ya nchi nyingine.

Ripoti zinaeleza kuwa mwanaume huyo hapo awali alikuwa akiishi nchini Uingereza kwa muda wa miaka 20 akiwa na marafiki na wanafamilia na hakuwa na historia ya kuugua ugonjwa wowote unaojulikana wa neva au ama akili.

Wataalamu wa afya nchini Marekani wamesema, wamewahi kukutana na wagonjwa kadhaa wa namna hiyo kwa vipindi tofauti huku ugonjwa huo wa FAS ukiwa ni kisa cha kwanza kumpata mtu mwenye tezi dume na kingine kikiwa ni cha mtu mwenye saratani.