‘Blueticks’ kulipiwa

0
251

Wapenda mitandao ya kijamii na watu mashuhuri wengi wamefikia nafasi ya kuwa na wafuasi wengi na maudhui yanayopendwa na wengi, hivyo kuwafanya kupata ‘verification’ ya tiki ya bluu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Meta Mark Zuckerberg ametangaza kuwa watumiaji wa mitandao ya Facebook na Instagram sasa wataanza kulipia kuzithibitisha kurasa zao kwa tiki ya bluu.

kupata ‘badge’ hiyo mtumiaji atalipa dola 11.99 za kimarekani kwa mwezi kwenye tovuti sawa na takribani TZS 28,056.60 na dola 14.99 za kimarekani kwa mwezi kwenye iOS ya Apple sawa na TZS 35,076.60.

Kama ilivyo kwa Twitter, watumiaji wenye tiki za bluu wataunganishwa na huduma ya moja kwa moja ya huduma kwa wateja.