Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Mhandisi Ladislaus Matindi amesema kwa sasa ni ndege tatu tu kati ya 11 mali ya shirika hilo ndizo zenye matatizo.
Amefafanua kuwa kati ya ndege hizo tatu, mbili zina kasoro za kiufundi kwenye injini
zulizotokana na mtengenezaji na moja ina tatizo la kisheria.
Mhandisi Matindi amewaambia waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam kuwa
ndege nane zingine zinaendelea kufanya safari katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na India na China.
“Tuna ndege nane zinazofanya kazi bila matatizo, zisizofanya kazi kwa matatizo ya kiufundi ni mbili, tatizo ni la watengenezaji, mnaweza kufuatilia kuhakikisha,” amesema Mhandisi Matindi na kuongeza kuwa “Kama mnataka kuhakikisha nendeni uwanja wa ndege, tena mkifika angalieni kwenye mkia ambako kuna namba imeanzia 5h kisha angalia namba.”