Dkt. Malasusa : Mchungaji Kimaro umesamehewa

0
145

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ( KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dkt. Alex Malasusa amesema kwa niaba ya kanisa amemsamehe
Mchungaji wa kanisa hilo ushariki wa Kijitonyama, Eliona Kimaro ambaye hivi sasa yuko kwenye likizo ya siku 60.

Askofu Malasula ametoa kauli hiyo wakati wa Ibada ya Jumapili katika kanisa la KKKT usharika wa Kinyerezi, Dar es Salaam.