Watuhumiwa wa ujambazi wauawa

0
139

Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira katika kitongoji cha Kilimahewa mamlaka ya mji mdogo wa Katoro mkoani Geita, baada ya kutuhumiwa kumuua Renata Elias ambaye alikuwa mjamzito wa miezi saba.

Mmoja wa watuhumiwa hao wa ujambazi waliouawa ni mtoto wa Msafiri Renatus ambaye nyumba yake ilivamiwa na majambazi hao na mke wake kuuawa kwa kuchomwa na visu.

Katika tukio hilo Renatus
ambaye ni baba wa familia hiyo iliyovamia amejeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwili wake.

Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Geita, Cornel Magembe amefika eneo la tukio na kutoa pole kwa wafiwa na kuliagiza jeshi la polisi wilayani humo kuzidisha doria ili kuwabaini watu wote wanaofanya vitendo vya uhalifu.

Magembe amewataka wale wote wenye nia ya kufanya vitendo vya uhalifu wilayani Geita kuachana na mpango huo, kwa kuwa mkono wa sheria utawanasa popote walipo..