Ngoma mpya ya AKA yaachiwa

0
241

Wimbo wa mwisho wa Rapa Kiernan Jarryd Forbes maarufu AKA wa Afrika Kusini aliyefariki dunia Februari 10 mwaka huu baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana umeanza kupigwa usiku wa kuamkia hii leo.

Familia ya AKA imesema, itaendelea kutoa kazi za Rapa huyo kama ilivyokuwa ikipaswa kufanyika akiwa hai na wapo mbioni kuachia albamu yake yenye jina la Mass Country kama ilivyopaswa kufanyika tarehe 24 mwezi huu.

Wimbo huo mpya wa AKA ulioachiwa usiku wa kuamkia hii leo “Company”, amemshirikisha nyota wa Nigeria KDDO ambaye alishirikiana naye hapo awali kwenye albamu ya “Touch My Blood” ya mwaka 2018 wimbo wa “Fela In Versace”.

Hadi sasa wimbo huo kwenye ukurasa wa AKA wa YouTube umeangaliwa zaidi ya mara laki tatu na nusu.

Hapo jana AKA alifanyiwa ibada ya kumuaga huko Sandton, Johannesburg na anazikwa leo katika jimbo la Gauteng, Afrika Kusini.