Nyoni aongezwa Stars

0
464

Mlinzi nguli wa timu ya Simba, -Erasto Nyoni ameongezwa kwenye kikosi cha wachezaji wa timu ya Taifa ya soka (Taifa Stars) iliyoingia kambini kujianda na mchezo wa mwisho wa kufuzu kwa michuano ya Afrika dhidi ya Uganda.

Nyoni ameongezwa na kocha Emmanuel Amonike ili kuziba nafasi ya mlinzi wa Yanga, -Andrew Vicente Dante ambaye ni majeruhi.

Mlinzi huyo wa Simba mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani, alikuwa nje ya dimba kwa kipindi cha miezi mitatu akiuguza majeraha.

Mchezo wa hivi karibuni wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika  kati ya Simba na AS Vita ya Kongo ulikuwa wa kwanza kwa Nyoni, na kiwango alichoonyesha kwenye mchezo huo kimemfanya aitwe tena kwenye kikosi cha Taifa Stars.

Taifa Stars inaanza mazoezi hii leo kujiwinda na mchezo huo dhidi ya Uganda ambapo inalazimika kushinda ili kufuzu kwa michuano ya Mataifa ya Afrika kwa mara ya pili baada ya kupita miaka 39.

Tayari baadhi ya wachezaji wanaocheza soka nje ya nchi wameshawasili nchini akiwemo winga Simon Msuva anayecheza soka nchini Morocco na wengine wanatarajiwa kuwasili hii leo na kesho.

Taifa Stars ni ya pili kwenye kundi lake la  L ikiwa na ina pointi Tano sawa na Lesotho na inaweza kufuzu kwenye michuano hiyo mikubwa kama itashinda mchezo huo huku ikiomba Cape Verde iizuie Lesotho.