Vijana 170 waanza mafunzo mradi wa EACOP

0
241

Kamishna wa mafuta na gesi nchini Michael Mjija amesema,
mradi wa ujenzi wa bomba la Mafuta Ghafi Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania upo na unaendelea kwa kufuata taratibu za ujenzi wa viwango vya kimataifa.

Mafunzo yanayotolewa ni ya utunzaji wa mazingira, usalama mahala pa kazi pamoja na afya na yanafanyika kwenye chuo cha ufundi Stadi cha VETA jijini Tanga.

Baadhi ya vijana ambao wameishapata mafunzo ya aina hiyo wamesema wapo tayari kufanya kazi, huku wakiahidi kuwa suala la usalama mahala pa kazi ndio kipaumbele chao.

Bomba la mafuta ghafi hapa nchini linapita katika mikoa 8,wilaya 24, kata 134 na vijiji zaidi ya 180 na wenye dhamana ya kuratibu shughuli zake hapa nchini ni Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Ujenzi wa mradi huo unafanyika kwa muda wa miezi 36 kwa gharama ya zaidi ya shilingi trilioni 11.