Mtoto wa Rihanna ndani ya Vogue

0
303

Mtoto wa kiume wa waimbaji maarufu Robyn Rihanna Fenty maarufu Rihanna na Rakim Athelaston Mayers maarufu A$AP Rocky wa nchini Marekani, anaungana na wazazi wake kwenye ‘cover’ ya jarida maarufu la British Vogue la mwezi Machi.

Picha hizo zinakuwa ni za kwanza za mtoto huyo mwenye umri wa miezi tisa, tangu Rihanna alipomwonesha kwa mara ya kwanza kwenye video ya Tiktok mwezi Desemba mwaka 2022.

Rihanna na A$AP Rocky ambao wana umri wa miaka 34 kila mmoja, walifanikiwa kupata mtoto huyo Mei 13 mwaka 2022, lakini mpaka sasa hawajaweka hadharani jina lake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Rihanna amemshukuru Mhariri Mkuu wa jarida hilo la British Vogue na mpigapicha wa jarida hilo.

Mwimbaji huyo maarufu wa “Diamonds”, hivi karibuni ameweka wazi kuwa yeye na A$AP Rocky wanatarajia kupata mtoto wa pili.