Barcelona yasitisha kuchapisha jezi namba 10

0
239

Klabu ya Barcelona imeamua kutochapisha tena jezi namba 10 ambayo alikuwa akiivaa Lionel Messi, kutokana na mchezaji anayevaa jezi hiyo kwa sasa Ansu Fati kukumbwa na changamoto ya jezi yake kutokuuzika katika klabu hiyo.

Itakumbukwa Lionel Messi tangu kuondoka katika klabu ya Barcelona mauzo ya jezi hiyo yamekuwa chini ikilinganishwa na awali ambapo alikuwepo klabuni hapo.

Hii inakuwa changamoto kwa Ansu Fati ambaye atalazimika kuongeza juhudi ili kuhakikisha angalau anafikia hata nusu ya kile ambacho alikuwa akikifanya Messi.

Kwa sasa jezi hiyo inatoka kwa oda maalum ambapo mtu anayehitaji jezi namba 10 ya Barcelona analazimika kutoa taarifa kwa uongozi ili kuchapishiwa.