Marc Anthony kupata mtoto wa 7

0
218

Mwanamuziki nguli wa miondoko ya Salsa kutoka nchini Marekani, Marc Anthony (54) na mkewe Nadia Ferreira (23) ambao wamefunga ndoa wiki mbili zilizopita, jana wametangaza kuwa wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza.

Marc Anthony ambaye hii ni ndoa yake ya nne anatarajia kupata mtoto wa 7 na mrembo huyo ambapo watoto wengine 6 amezaa na wake zake watatu.

Mwimbaji huyo na mke wake wamechapisha picha zinazoonesha ujauzito huo kwenye mitandao ya kijamii na kuandika ujumbe wa kuhusisha furaha waliyonayo na siku ya wapendanao.

Baadhi ya wakosoaji walipinga hatua ya Marc Anthony kumuoa Nadia ambaye ana umri mdogo wakilinganisha na wa binti yake wa kwanza mwenye miaka 29.