Tatizo la umeme mjini na vijijini lapatiwa muarobaini

0
176

Waziri wa Nishati January Makamba amesema serikali imeamua kuanza utekeledaji wa miradi ya kuimarisha gridi ya Taifa ili kuimarisha miundombinu na mitambo ya usafirishaji umeme na kuondokana na changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara.

Ameongeza kuwa wizara ya Nishati imetumia madhaifu yaliyobainishwa kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2019 ikitaja miundombinu chakavu na matengenezo hafifu ya mitambo ya umeme na kuamua kufanya maboresho.

Kwa upande wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mkurugenzi Mkuu wa wakala huo Hassan Said amesema, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamesaini mikataba ya kukamilisha miradi yake mitatu mikubwa iliyotiliwa saini hii leo Ikulu, Dar es Salaam.