Mashirika ruksa kuajiri

0
269

“Kuna mashirika ambayo wenyewe wangehitaji ajira za harakaharaka lakini unaambiwa subiri Tume ya Utumishi ikae, subiri sijui utumishi ifanyeje mwaka mzima taasisi kwa mfano TRA inataka watu wakakusanye mapato mwaka mzima watu hawajapatikana, vivyo hivyo TANESCO, REA wanataka watu utumishi paka izunguke iseme ifanye mikutano ifanye semina, hapana hatuendi hivyo.

Kama wanataka wafanyakazi mishahara ya kulipa wanayo haitoki hazina wanataka wafanyakazi kwa ajili ya mradi au kazi fulani wapewe ruhusa wafanye. Wapewe ruhusa wafanye sabahu ajira hizi wala nyingine sio za kudumu mradi ukimalizika na ajira imekwenda. Kwa hiyo wapewe ruhusa waajiri ili miradi ikatekelezwe kwa haraka.”

Rais Samia Suluhu Hassan