Wanapokosa mradi fitna nyingi

0
106

“Uchaguzi au uteuzi wa wakandarasi hawa umefanywa kwa umakini mkubwa sana. Natambua kuna wenzetu wengine kila mtu alikuwa na mkandarasi wake mkononi na alipenda apate, kwa sababu hakupata fitina ni nyingi. Mbio PPRA mbio PCCB mbio sijui wapi, nenda kule mradi usifanyike uzuie kwa matakwa yake binafsi, hatutakwenda hivyo.

Ili miradi hii ifanyike haraka, ili tupate maendeleo ya haraka tunahitaji maamuzi ya haraka. Unapokosa ukaenda PCCB ukaenda PPRA unazuia miradi kutofanyika na unazuia utendaji kwenda kwa haraka na wale wenye taasisi hizi pimeni ndugu zangu mnacholetewa sio mtu kakosa yeye tenda mbio anakuja kwenu kila kitu kinasimama, hapana.”

Rais Samia Suluhu Hassan