Watuhumiwa wa wizi mbaroni Kasulu

0
450

Watu 17 wakiwemo Watanzania Watatu na Wakimbizi 12 kutoka kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma wanashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kukutwa na magunia zaidi ya 600 ya njegere yanayodaiwa kukusanywa kinyume cha sheria kwa Wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu.

Mkuu wa wilaya ya Kasulu, – Kanali Simon Anange amesema kuwa watu hao wamekamatwa baada ya kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo kupata taarifa ya uwepo wa biashara haramu ya vyakula vinavyogawiwa kwa wakimbizi na hivyo kuamua kuweka mtego.

Kanali Anange amedai kuwa baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi waliopo ndani na nje ya kambi hiyo, pamoja na watendji wa mashirika yanayohudumia wakimbizi ni miongoni mwa wahusika wa mtandao huo wa wizi wa vyakula vinavyogawiwa kwa Wakimbizi.