Ujumbe wa Tanzania wawasili Italia

0
247

Ujumbe wa mawaziri wawili na katibu wakuu wawili wa Tanzania Bara na Zanzibar kutoka Wizara za Uvuvi na Mifugo, pamoja na ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi umewasili leo Jumapili Februari 12 mjini Roma nchini Italia tayari kushiriki Baraza Kuu la Mfuko wa Maendeleo ya Chakula na Kilimo duniani (IFAD) unaotarajiwa kuanza kesho.

Ujumbe huo umewajumuisha Waziri Mashimba Ndaki na viongozi wenzake waliopokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Balozi Mahmoud Thabit Kombo pamoja na maafisa wa ubalozi huo wakiongozwa na Mwambata wa Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Misitu, Jacquiline Mhando.