Simba SC yachezea kichapo Guinea

0
264

Simba SC imepoteza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika ikiwa ugenini dhidi ya Horoya AC ya nchini Guinea.

Simba ilifungwa goli la mapema ambalo limedumu hadi mwisho wa mchezo, huku sifa zaidi zikienda kwa Aishi Manula baada ya kupangua mkwaju wa penati.

Baada ya kupoteza mchezo huo, sasa Simba inarudi nyumbani kujiuliza kwa kwa Raja Casablanca ya Morocco ambayo ilipata ushindi wa magoli 5-0 katika mchezo wake wa kwanza ikiifunga Vipers SC ya Uganda.

Baada ya michezo ya kwanza, Raja Casablanca inaongoza kundi ikiwa na idadi kubwa ya magoli ikifiatiwa na Horoya AC, kisha Simba ikiwa kwenye nafasu ya tatu na mkiani ipo Vipers SC.

Je! ni timu zipi (mbili) zitafuzu hatua ya makundi? baada ya mechi sita kwa kila timu, jibu litakuwa hadharani.