Mbeya kuendelea kunufaika na miradi ya maji

0
175

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema mkoa wa Mbeya utaendelea kunufaika na miradi ya maji na kumtua mama ndoo ya maji kichwani kama ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inavyoeleza.

Waziri Aweso ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa utekelezaji mradi wa maji kutoka chanzo cha Mto Kiwira mkoani Mbeya.

Katika hotuba yake Aweso amesema amepokea maombi ya mkuu wa mkoa wa Mbeya, Juma Homera ya kutaka kijiji cha Itumbi kilichopo kata ya Matundasi wilaya ya Chunya kufikishiwa maji safi na salama.

Mradi wa maji kutoka chanzo cha mto Kiwira  utakapokamilika unatarajiwa kuzalisha maji kutoka lita milioni 66 hadi  kufikia lita milioni 84 kwa siku na kuweza kuwafikia wananchi wapatao milioni 1.4.

Awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huo itakamilika kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia tarehe 25/2/ 2023 hadi 24/2/2025.