Bilioni 99 kumaliza kero ya maji Mbeya

Mradi wa Maji

0
216

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa baadhi ya maeneo mkoani humo inakwenda kumalizika, baada ya serikali kutangaza utekelezaji rasmi wa mradi wa maji wa mto Kiwira.

Homera ameyasema hayo wakati wa mahojiano na TBC na kuongeza kuwa, mradi huo utagharimu shilingi bilioni 99 na kuzalisha zaidi ya lita mia mbili za maji kwa siku.

Makubaliano ya utekelezaji wa mradi huo yatasainiwa hapo kesho, ambapo Waziri wa Maji Jumaa Aweso anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.