Arteta: Jesus ameanza mazoezi mepesi

0
385

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amethibitisha kuwa Gabriel Jesus ameanza mazoezi ya nje akisubiriwa kwa hamu kurejea kikosini baada ya kukaa nje kwa takribani miezi mitatu.

NINI KILITOKEA? Mshambuliaji huyo raia wa Brazil aliumia goti wakati akiitumikia nchi yake katika mashindano ya Kombe la Dunia nchini Qatar mwishoni mwa mwaka 2022.

HALI IKOJE? Nyota huyo tegemezi aliyejiunga na washika bunduki wa London msimu wa kiangazi amerejea klabuni hapo akiendelea na mazoezi kama sehemu ya matibabu.

ARTETA AMESEMAJE? Akizungumzia mchezo wa Jumamosi dhidi ya Brentford, ametoa taarifa ya kutia moyo. “Gabi anaendelea vizuri sana, tayari ameanza kutoka nje,” amesema Arteta kuhusu nyota huyo mwenye miaka 25.

Licha ya taarifa hiyo amesema itamchukua muda kidogo kupona na kurejea kikosini.

HALI YA KIKOSI? Amesema wachezaji wengine wenye majeraha ambao ni Emile Rowe (paja) na Reiss Nelson (kifundo cha mguu) wanaendelea vizuri na mazoezi ya viungo lakini bado hawako tayari kurejea kikosini.

Arsenal wanauwinda ushindi dhidi ya Bretford ili kurejesha morali ya ushindi na kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa, baada ya kupoteza mchezo uliopita.