Boeing 737 MAX 8 na 9 marufuku Rwanda

0
565

Shirika la Ndege la Rwanda (RCAA) limewaagiza marubani wote na kampuni zote za ndege nchini humo kutoendesha ndege za Boeing 737 MAX 8 na 9 katika anga ya nchi hiyo.

Rwanda inaungana na mataifa mengine duniani ambayo yamepiga marufuku usafiri wa ndege hizo za aina ya Boeing 787 MAX 8 na MAX 9.

Hatua hiyo ya Rwanda na mataifa mengine, inafuata ajali ya kuanguka kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia muda mfupi baada ya kupaa kutoka mji mkuu Addis Ababa kuelekea Nairobi, -Kenya na kusababisha vifo vya watu wote 157.

Taarifa zaidi zinasema kuwa Rwanda ilikuwa na mpango wa kukodi ndege mbili aina ya Boeing 737 MAX 8, lakini kwa sasa mpango huo umesitishwa kwa muda ili kusubiri uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo ya ndege ya Ethiopia.

Ndege kama hiyo, mali ya kampuni ya Lion Air, ilianguka katika Pwani ya Indonesia mwezi Oktoba mwaka 2018 na kusababisha vifo vya watu wote 189.