Domenico Tedesco Kocha mpya Ubelgiji

0
169

Kocha wa zamani wa Schalke, Spartk Moscow na RB Leipzig, Domenico Tedesco ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya Taifa ya Ubelgiji kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Roberto Martinez.

Domenico Tedesco (37) mzaliwa wa Italia mwenye uraia wa Ujerumani amesaini kandarasi ya kuinoa timu hiyo hadi kwenye michuano ya Euro ya 2024.

Roberto Martinez aliinoa Ubelgiji kwa muda wa miaka sita na alitolewa kwenye hatua ya makundi kwenye michuano iliyopita ya kombe la Dunia kule nchini Qatar na akajiuzuru na sasa ni kocha wa Ureno.

Kocha huyo kijana amesema ni jambo jema kwake kupewa nafasi hiyo ya kuinoa timu ya Taifa ya Ubelgiji na yuko tayari kwa changamoto mpya za kazi hiyo ya kuinoa timu ya Taifa ya Ubelgiji.

Kibarua cha kwanza cha kocha huyo kitakuwa mchezo wa kufuzu kwa michuano ya Euro 2024 dhidi ya Sweden mjini Stockholm Machi 24 mwaka huu.