Asilimia 97 ya namba za simu zimehakikiwa

0
186

“Nichukue hatua hii kushukuru wananchi kwa sababu hadi kufikia tarehe 5, juzi, tuna jumla ya laini milioni 60.6 ambazo zimesajiliwa kwa alama za vidole, lakini kati ya hizo, laini milioni 58.7 hizi zimekwishahakikiwa hii ni sawa na asilimia 97.
Laini ambazo hazijahakikiwa mpaka tarehe 5 juzi ni milioni 1.9, kama asilimia tatu hivi.

Ambao hawajahakiki kwa hesabu rahisi ni kwamba kwa kila laini 100, watu 97 wamekwishahakiki kwa hiyo tuna watu watatu tu kati ya watu 100 ambao hawajahakiki na hao ndio ambao tunawasihi kwa siku zilizobaki basi wafanye uhakiki.”

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri Bakari