Vilio vyatawala wakati wa kuaga miili 12

0
174

Shughuli ya kuaga miili ya watu 12 waliofariki dunia katika ajali ya gari wilayani Korogwe mkoani Tanga inaendelea hivi sasa katika viwanja vya hospitali ya Huruma wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, ambapo
mkuu wa mkoa huo Nudrin Babu amewaongoza waombolezaji kuaga miili hiyo.

Habari zaidi kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa, vilio vimetawala wakati wa shughuli ya kuaga miili hiyo huku ndugu, jamaa na marafiki wakishindwa kujizuia huzuni zao.

Watu hao 12 ambao ni wanafamilia, ni miongoni mwa watu 17 waliofariki dunia katika ajali hiyo.

Walikuwa wakisafirisha mwili wa Athanas Mrema kutoka mkoani Dar es Salaam kwenda Rombo kwa ajili ya mazishi.