“Tutaanza kuvuna kuanzia mwezi wa nne na sisi kama serikali kuanzia mwaka ujao wa fedha tutaanza kununua mpunga na mahindi ya kutosha tutahifadhi na kuongeza uwezo wetu wa kuhifadhi katika maghala ya serikali kwa kiwango kisichopungua tani laki tano ili pale tunapokuwa na shida za namna hii tuweze kutoa chakula kingi na kiingie sokoni.
Nataka niwaambie wafanyabiashara kama wewe umefungia mchele na mahindi ndani serikali inafungua pampu hivi karibuni ni heri uyawahishe sokoni upate faida yako na tutaanza kuuza mahindi kwa bei isiyozidi shilingi mia saba au mia nane kwa kilo.”
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe