Chongolo asisitiza usimamizi rasilimali za maji

0
138

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo ameiagiza Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu kuongeza kasi katika usimamizi wa rasilimali za maji kwa kupanda miti kwenye maeneo ambayo yameshaanza kuharibiwa na shughuli za kibinadamu.

Chongolo ametoa agizo hilo mjini Morogoro baada ya kuzindua vitalu vya miche ya miti itayopandwa katika maeneo yote ya pembezoni mwa mito ndani ya bonde hilo.

Katibu Mkuu huyo wa CCM Taifa leo anahitimisha ziara yake ya siku tisa mkoani Morogoro kwa kushiriki maadhimisho ya miaka 46 tangu kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi.