Shambulio la kigaidi lasababisha vifo vya watu 40

0
564

Watu Arobaini wameuawa na wengine zaidi ya Ishirini wamejeruhiwa, baada ya kutokea kwa mashambulio katika misikiti miwili kwenye mji wa Christchurch, huko New Zealand.

Waziri mkuu wa New Zealand, – Jacinda Ardern amelitaja shambulio hilo kuwa ni la kigaidi.

Tayari watu watatu wamekamatwa kwa tuhuma za kupanga mashambulio hayo.

Jeshi la Polisi katika mji huo wa Christchurch limesema kuwa watu hao waliokamatwa hawamo kwenye orodha ya magaidi wanaotafutwa, lakini wamekamatwa kutokana na kuwa na itikadi kali.

Waziri mkuu wa Australia, -Scott Morrison amesema kuwa mmoja wa watu waliokamatwa ni raia wa nchi hiyo.