Ndege ya Precision yatua kwa dharura

0
172

Shirika la Ndege la Precision Air limethibitisha kuwa ndege zake mbili zimeshindwa kufanya safari zake kama kawaida baada ya ndege moja kupata hitilafu na nyingine kulazimika kutua kwa dharura.

Kupitia taarifa yake shirika hilo limesema moja ya ndege zake ilipata hitilafu ya kiufundi hivyo kusababisha kuchelewa na kuahirishwa kwa safari na nyingine ililazimika kutua kwa dharura baada ya kugonga kiumbe aina ya ndege wakati ikiruka kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma.