Sheikh Alhad aondolewa Dar

0
216

Baraza la Ulamaa katika kikao chake kilichofanyika kwa muda wa siku mbili mkoani Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake Multi wa Tanzania Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally, limetengua uteuzi wa Sheikh Alhad Mussa Salum kama Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam kuanzia leo Februari 02, 2023.

Wakati huo huo Mufti amemteua Sheikh Walid Alhad Omar kukaimu nafasi ya Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam kuanzia leo Februari 02, 2023.