Nasari avuliwa Ubunge

0
439

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungana wa Tanzania Job Ndugai amemuandika barua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Semistocles Kaijage kuwa Jimbo la Arumeru Mashariki kwa sasa liko wazi.

Jimbo hilo liko wazi kufuatia Mbunge wake Joshua Nasari kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) kushindwa kuhudhuria mikutano mitatu mfululizo na hivyo kupoteza sifa za kuendelea kuwa mbunge.