Wafanyabiashara wakimbia soko la Bwawani

0
143

Licha ya serikali kuwekeza shilingi bilioni 1.2 katika mradi wa ujenzi wa soko la bwawani lililopo manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, wafanyabiashara wamelikimbia soko hilo kwa madai ya kukosekana kwa wateja.

Manispaa ya Kinondoni kupitia mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP), imewekeza kiasi hicho cha fedha ili kuwanufaisha wakazi wanaoishi Bwawani na maeneo jirani.

Baadhi ya wafanyabishara waliobaki katika soko hilo la Bwawani
wamedai kuwa kukosekana kwa wateja na uwepo wa magenge pembezoni mwa soko hilo ni chanzo cha kulikimbia na kwenda kujitafutia rizki maeneo jirani.

Wamesema uwepo wa magenge pembezoni mwa soko hilo la Bwawani na maeneo jirani kunasababisha wateja kununua bidhaa katika magenge hayo na kuliacha soko.

Wemeiomba serikali kuanzisha minada ambayo itachochea wateja na wafanyabiashara kuwa na mazoea ya kupata huduma sokoni hapo pamoja na kuwepo kwa huduma ya usafiri wa daladala kupita sokoni hapo.

Soko la Bwawani lina jumla ya vizimba 153 na maduka 29 ambayo yote yamepata wapangaji isipokuwa wengi wao wamelikimbia soko hilo na kuacha maeneo yao wazi.