DMDP na suluhu ya mafuriko mto Ng’ombe

0
128

Mafuriko yaliyokuwa yakitokea mara kwa mara katika mto Ng’ombe na kuathiri maeneo ya Sinza, Tandale kwa Mtogole, Mwananyamala Kisiwani, Kijitonyama mpakani na maeneo mengine ambayo mto huo unapita kwa sasa yamekuwa historia, kufuatia kukamilika kwa mradi wa ujenzi katika mto huo.

Mradi huo unaohusisha ujenzi wa mabwawa mawili ya kupunguza kasi ya maji, kingo za mto
zenye urefu wa kilomita 8.5, vivuko 15 na madaraja manne umegharimu shilingi bilioni 32.5.

Wakazi wa maeneo hayo wameishukuru serikalli kwa kuwapelekea mradi huo ambao umetoa suluhisho la kudumu kutokana na mafuriko hayo yaliyokuwa yakitokea mara kwa mara.

Wamesema kabla ya ujenzi wa mradi huo walikuwa wakikumbana na adha ya mali zao kusombwa na mafuriko ambayo pia yalikuwa yakibomoa nyumba zao, watu kufariki dhnia na watu kuyahama makazi yao.

Mradi huo wa ujenzi wa mto ng’ombe, ni miongoni miradi ya awamu ya kwanza inayotekelezwa na mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Jiji la Dar es Salaam (Dar es Salaam Metropolitan Development Project – DMDP) katika wilaya ya Kinondoni.