Usuluhishi kuchochea uwekezaji

0
265

Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali imedhamiriaa kukuza uchumi kwa kufungua fursa za uwekezaji na biashara ambazo zina ushindani, ambapo masuala mengi yanayotokea yanahitaji usuluhishi.

Rais Samia ameyasema hayo mkoani Dodoma wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini.

Dkt. Samia ameongeza kuwa Tanzania imefunguliwa kuwa kitovu cha biashara ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambapo wawekezaji wanazidi kuvutiwa kila zinapofanyika ziara za viongozi nje ya nchi.

Amesema kutokana na hilo, wawekezaji wote wanaokuja nchini wanataka kuona haki ikitendeka wanapofanya biashara na kuwekeza mitaji yao.

Rais Samia amesema ni muhimu kuimarisha mifumo ya utoaji haki ili iweze kutatua migogoro kwa haraka pale inapotokea, hali itakayowavutia wafanyabishara na wawekezaji kwa kuwa inalenga imani ya usalama wa mali zao.