Halmashauri zatakiwa kuanzisha miradi ya maendeleo

0
348

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo amewaagiza wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa halmashauri na majiji  nchini kuhakikisha fedha za mapato zinazokusanywa kwenye maeneo yao  zinatumika kuanzisha miradi ya maendeleo ya wananchi na si kwenye matumizi mengine ya ofisi.


Waziri Jafo ametoa agizo hilo  mkoani Kigoma wakati akizindua mradi wa  kuunganisha mfumo wa Ukusanyaji wa Mapato (LGICIS) na ule wa Taarifa za Kijiografia (GIS) na kuelezea kutofurahishwa na kitendo cha baadhi ya halmashauri  nchini  kutenga fedha ndogo ya mapato  kwenye miradi ya maendeleo.


Aidha waziri Jafo ameitaka Manispaa ya Kigoma, -Ujiji kutumia mfumo wa LGICIS ili kuratibu mienendo ya kusanyaji wa mapato  kwenye vyanzo vyake, lengo likiwa ni kuongeza kiwango cha mapato ya Manispaa hiyo ambayo kwa muda mrefu imekuwa haifanyi vizuri.


Mradi wa  kuunganisha mfumo wa ukusanyaji wa mapato (LGICIS) na ule wa taarifa za Kijiografia (GIS) unatekelezwa  katika majiji Matano na Manispaa Tatu nchini.