Murtaza Mangungu ametangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya uenyekiti wa klabu ya Simba kwa mara nyingine tena, kufuatia uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika mkoani Dar es Salaam.
Mangungu ametetea nafasi hiyo kwa kupata kura 1,311 dhidi ya Moses Kaluwa aliyepata kura 1,045.
Wajumbe Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo ya Simba waliochaguliwa ni Dkt. Seif Muba aliyepata kura 1,636, Asha Baraka aliyepata kura 1,564, Issa Masoud aliyepata kura 1,285, Rodney Chiduo aliyepata kura 1,267 na Seleman Harubu aliyepata kura 1,250.