Rais asherekea siku ya kuzaliwa na watoto yatima

0
195

Rais Samia Suluhu Hassan leo amesherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutoa zawadi na pesa taslimu katika vituo saba vya watoto yatima.

Vituo hivyo saba vimekabidhiwa zawadi hizo na Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega kwa niaba ya Rais Samia.

Makabidhiano ya zawadi hizo yamefanyika katika kituo cha Children Home Msimbazi kilichopo Ilala mkoani Dar es Salaam ambapo pia Naibu Waziri Ulega alipata fursa ya kutembelea na kuwajulia hali watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho.

Kituo kingine kilichokabidhiwa zawadi hizo ni kile cha watoto cha Mburahati.

Zawadi zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa vituo hivyo vya watoto yatima ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa
ni pamoja na pempasi za watoto, unga, sabuni, sukari, maziwa na mafuta.

Vituo vingine vya watoto yatima ambavyo vimepelekewa zawadi hizo ni Tua Ngoma, Mbagala, Mbweni, Mwasonga na Sinza.