Msanii Peter Msechu ni miongoni mwa watu waliopatiwa matibabu ya kuwekewa puto tumboni (intragastric balloon) katika hospitali ya Mloganzila, Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Mohamed Janabi amesema,
matibabu hayo ya kuwekewa puto tumboni yanasaidia kupunguza uzito kwa
watu wenye uzito wa zaidi ya kilo 90 ambapo Msechu ana kilo 144.