Simba SC yapata mrithi wa Barbara

0
184

Simba SC imemuajiri Imani Kajula kuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) kwa mkataba wa miezi sita akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Barbara Gonzalez ambaye alijiuzulu Desemba 10, 2022.

Katika taarifa yake Simba imesema kuwa Kajula ni mzoefu kwenye masuala ya uongozi wa mpira kwani alikuwepo kwenye Kamati ya Maandalizi ya Michuano ya Afrika kwa Vijana chini ya miaka 17 iliyofanyika nchini mwaka 2019.

Kabla ya kujiunga na Simba SC alikuwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Masoko na Mawasiliano ya EAG Group tangu mwaka 2013.