Man United yaikaribia fainali ya Carabao Cup

0
204

Manchester United inaikaribia fainali ya Carabao-Cup baada ya kushinda mchezo wa kwanza wa nusu fainali dhidi ya mabingwa mara nne wa kombe hilo, Nottingham Forest.

Mashetani Wekundu wamepata ushindi mnono wa magoli 3-0 wakiwa ugenini magoli yakifungwa na Marcus Rashford dakika ya 6, Wout Weghorst dakika ya 45 kabla ya kiungo Bruno Fernandes hajakamilisha karamu hiyo dakika ya 89.

Ushindi wa mchezo unaofuata utaipeleka Mancherster United katika dimba la Wembely ikikusudia kumaliza ukame wa makombe unaoiandama, ikikumbukwa kuwa mara ya mwisho kushinda kombe ni mwaka 2017, huku pia ikikumbuka kupoteza fainali ya Kombe la Shirikisho (FA Cup) mwaka 2018.

Rashford anaendelea kuwa na msimu mzuri tangu kumalizika kwa Kombe la Dunia akifunga goli katika michezo 10 mfululizo ya Manchester.